Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
KITUO
cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for
Agricultural and Rural Cooperation, CTA) kilicho chini ya Umoja wa Ulaya
(EU) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais
Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador)
wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Caribean na Pacific.
Katika
barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora,
CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,
ameteuliwa kwa kutambua mchango na juhudi zake katika kukiendeleza
kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.
Katika
wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha
katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umuhimu wa
kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha na
uhakika kwa vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani
na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya
mahojiano na waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.
Dk.
Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika
kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidiana na taasisi hiyo ambayo ni
ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani
na Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelgiji.
Prof.
Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya
CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano
tangu 2013 hadi 2018
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni