Jumatano, 15 Februari 2017

WATANZANIA KUFUKUZWA MSUMBIJI: NI SHUKRANI YA PUNDA???




Juzi watanzania 58 ambao walikuwa wanaishi nchini Msumbiji wamefukuzwa nchini humo na kurudishwa Tanzania huku wakidai kunyang’anywa mali zao, vitambulisho pamoja na hati za kusafiria na askari wa Msumbuji.
Watanzania hao kabla ya kufikishwa kwenye mpaka wa Tanzania na Msumbiji mpaka wa Kilambo waliwekwa ndani ya mahabusu kwa siku tatu bila chakula.
Watanzania ambao wamefukuzwa nchini Msumbiji wamesena wameacha kila kitu, fedha walizokuwa nazo mifukoni wameporwa na askari wa Msumbiji wakati wanakamatwa, sehemu zao za biashara ambazo walikuwa wamefungua wameziacha wazi, bila kufuata taratibu raia hao waliwekwa mahabusu na baada ya siku tatu wakafikishwa mpaka wa Kilambo mkoani Mtwara ambao ni mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
Wakiwa mkoani Mtwara raia hao ambao wanatoka mikoa mbalimbali hapa nchini wameiomba serikali kuwasaidia kwani hata mawasiliano na ndugu zao yamekuwa magumu kutokana kuporwa simu na askari wa Msumbiji.
Jambo la kujiuliza ni hili: Hii sio shukrani ya punda? 
Ikumbukwe kuwa Tanzania iliwasaidia Watu wa Msumbiji kwenye vita ya kumng'oa Mreno na baadaye katika vita dhidi ya RENAMO. Watanzania wengi walikufa kwenye vita hizo mbili. Wengi walipata ulemavu wa kudumu. Lakini pia Wareno waliua watanzania wengi pale walipokuwa wanashambulia Mkoa wa Mtwara  kama kulipiza kisasi kwa kitendo cha kuisaidia FRELIMO.
Cha kufanya tunao watu wengi wa Msumbiji hapa nchini. tunashauri Serikali makini ya awamu ya tano kuwarudisha makwao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni