Mwanamke ambaye
alichukuliwa kutoka kwa mama yake baada ya kuzaliwa nchini Argentina,
ameunganishwa na familia yake na kundi linalofahamika kama Grandmothers
of the Plaza de Mayo.
Adriana, 40, ambaye aliomba jina lake la pili kutofichuliwa alitambulia baada ya kufanyiwa uchunguzi wa DNA.DNA yake ililingana na ya familia ya wazazi wake ambao walitokeka wakati wa utawala wa kijeshi nchini Argentina.
Adriana ndiye mtoto wa 126 kupatikana na Grandmothers, ambao wanaendesha kampeni kwa niaba ya waathirika wa "Dirty War".
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari, Adriana alisema kuwa wakati watu waliokuwa wamemlea walikufa, aliambiwa na mtu mwingine kuwa yeye hakuwa mtoto wao wa kuzaliwa.
Alifanyiwa uchunguzi wa DNA na baada ya miezi minne hakupata DNA iliyolingana na yake, kutoka kwa ile inayohifadhiwa na Grandmothers ya watu waliotoweka au kuuawa na utawala wa kijeshi.
"Nilianza kufikiri kuwa nilitelekezwa, nilitolewa au kuuza kwa sababu hawakuwa wananitaka." alisema Adriana.
Lakini siku ya Jumatatu alipata simu kutoka tume ya kitaifa ya haki ya kutambuliwa, ikimuambia kuwa walikuwa na ujumbe wangependa kumpa.
Adriana alienda mara moja na kuambiwa kuwa alikuwa binti wa Violeta Ortolani na Edgardo Garnier, wote waliotoweka wakati wa utawala wa kijeshi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni