Jumanne, 5 Desemba 2017

Mwigizaji nyota wa Bollywood Shashi Kapoor afariki dunia

Shashi Kapoor in his younger days

Shashi Kapoor aliigiza kwenye filamu zaidi ya 150
Mwigizaji mkongwe wa Bollywood Shashi Kapoor amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.
Kapoor, aliyeigiza katika filamu maarufu kutoka India kama vile Deewar na Kabhie Kabhie, amekuwa akiugua kwa muda na alikuwa amelazwa hospitali.
Shashi anatoka familia ya Kapoor ambayo imetawala tasnia ya filamu za Kihindi kwa miongo mingi.
Alishinda tuzo nyingi za filamu za taifa na alitunukiwa tuzo kuu ya heshima inayopewa raia na serikali ya India mwaka 2011, tuzo ya Padma Bhushan.
Aliigiza pia katika filamu kadha za Uingereza na Marekani.
Kapoor amefariki wakati akitibiwa katika hospitali ya Kokilaben Dhirubhai Ambani mjini Mumbai.
Mpwa wake Randhir Kapoor ameambia Press Trust of India kwamba Kapoor alikuwa na matatizo ya figo kwa miaka mingi.
 
Shashi Kapoor in his younger days
Shashi Kapoor alipokuwa kijana bado
Mwili wake utazikwa kesho asubuhi.
Alikuwa amemuoa mwigizaji mwingereza Jennifer Kendal, ambaye kwa pamoja walianzisha ukumbi maarufu wa sanaa Mumbai wa Prithvi mwaka 1978.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni