Jumatatu, 13 Oktoba 2014

KIJANA ACHEZEA KICHAPO BAADA YA FUMANIZI

Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Jose akivuja damu baada ya kipigo.Msala huo wa aina yake ambao ulivuta umati mkubwa ulijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Makumbusho jijini Dar baada ya kijana huyo kuwekewa mtego na kukutwa na mke wa mtu akimsomesha.

Adabu ishike mkondo wake! Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Jose amejikuta akichezea kichapo ‘hevi’ kilichomsababishia kuvunjika pua kwa tuhuma ya ukuwadi wa mke wa mtu, .
Kijana Jose akiondolewa eneo la tukio asije kuumizwa zaidi.Kwa mujibu wa jamaa waliomwekea mtego Jose (wa kwanza kulia pichani juu), jamaa huyo amekuwa sugu mtaani hapo kiasi cha kuwakera baadhi ya vijana wenye wapenzi na wake zao.Jose alishuhudiwa akila kichapo kutoka kwa vijana wasiotaka kufuata sheria bila shurti hadi akatiririkwa damu chapachapa puani baada ya kuvunjika pua.
Baadhi ya vijana bado wakiwa na gadhabu wakati wa kuamulizia ugomvi huo.
“Haiwezekani awe anawakuwadia wake zetu kwa wanaume wengine, leo tulipanga tumtoboe hata jicho moja ili liwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama za Jose,” alisema mmoja wa vijana waliokuwa wakimsulubu jamaa huyo.Vijana waliokuwa eneo la tukio wakizozana katika songombingo hilo.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mwanaume aliyemwekea mtego Jose ambaye aliomba hifadhi ya jina gazetini alisema kwamba, waliamua kumpa mkong’oto kijana huyo baada ya kuchoshwa na vitendo vyake hivyo.


Baadhi ya vijana wenye hasira waliochoshwa na tabia ya kikuwadi ya Jose. Alisema hata mkewe alishamuonya juu ya mazoea na Jose na kumweleza kuwa akimkuta tu na kijana huyo lazima atampa talaka jambo ambalo lipo kwenye ‘prosesi’.
Kwa upande wake Jose alishindwa kusema lolote huku akisikilizia maumivu ya kipigo hadi alipoondolewa eneo la tukio na wasamaria wema.

Jumatatu, 6 Oktoba 2014

RONALDO AWEKA REKODI YA HAT TRICK

10649779_808787392518541_1971687263503280706_n
Mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo jana usiku alifunga magoli matatu na kutimiza jumla ya magoli 17 katika michuano yote aliyoitumikia Real Madrid. Magoli hayo yalimfanya Ronaldo aweke rekodi kadhaa kwenye historia ya soka na rekodi hizo zipo kama ifuatavyo:

*3 – Hii ni Hat trick ya 3 ya Ronaldo katika La Liga msimu huu na amefanikiwa kufunga hat tricks hizo katika kipindi cha siku 15 tu.
*111 – Mchezo wa jana usiku ulikuwa wa 111 kwa Ronaldo kuitumikia timu yake ya taifa au klabu na katika mechi hizo zote amefunga zaidi ya goli moja.
*Cristiano amekuwa mchezaji wa pili kufunga hat tricks 3 katika mechi 7 za raundi ya kwanza ya La Liga – baada ya Mariano Martin kufanya hivyo msimu wa 1943-44.
*Cristiano ndio mchezaji wa kwanza kufunga magoli 13 au zaidi katika mechi 7 za kwanza Liga – tangu alipofanya hivyo Echevaria katika msimu wa 1943.
*50 – Cristiano Ronaldo mpaka sasa ameshatoa assists 50 kwa wachezaji wenzie wa Real Madrid.
*190 – Magoli matatu aliyofunga Cristiano Ronaldo jana dhidi ya Athletic Bilbao yalimfanya atimize jumla ya magoli 190 katika mechi 171 alizoichezea Real Madrid kwenye ligi.
*9 – Gareth Bale mpaka sasa amempa Cristiano Ronaldo assists nyingi kwenye La liga tangu mwanzo mwa msimu uliopita – amempata assists 9.

HITILAFU YA UMEME KIJANA ANUSURIKA KIFO ANAHITAJI MSAADA WAKO

Kijana  Saadam Hussein aliyeunguzwa
KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Saadam Hussein (14), mkazi wa Chanika nje kidogo ya jiji la Dar es Slaam amelalamikia umeme kubadili sura yake baada ya kuungua vibaya na moto uliosabishwa na hitilafu ya nishati hiyo katika nyumba yao iliyotokea wiki mbili zilizopita.
Kijana huyo aliungua vibaya kutokana na hitilafu ya umeme. Akizungumza na gazeti hili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji, baba wa kijana huyo Hussein Ally alisema mtoto wake anayelala katika chumba karibu na dukani, alisikia vitu vikidondoka, lakini alipojaribu kuamka, akakutana na moto huo ukiwa umekolea.
Alisema kijana wake alitaka kuokoa mali zilizokuwa zinateketea na moto, lakini moshi na ukali wa moto ulimzidi nguvu na kusabisha kushindwa kuona na hivyo kuungua huku duka lote likiteketea. Alisema pamoja na mali zote zilizokuwepo dukani kuteketea, lakini pia mauzo ya siku 9 yanayokadiriwa kufikia shilingi milioni 1.9 nayo yaliungua. “Kijana wangu ameungua vibaya sana, hapa ninamuomba Mungu tu maana hata kuongea ni shida,” alisema baba huyo kwa huzuni.
Muuguzi aliyekuwa zamu, ambaye alikataa kutaja jina lake kwa vile siyo msemaji wa hospitali hiyo, alisema kijana huyo ameungua vibaya, ingawa bado hawajajua ni kwa asilimia ngapi

Saadam Hussein akiwa na Baba yake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Kuna viwango cha kuungua, siwezi kujua ameungua kwa asilimia ngapi lakini sehemu kubwa ya mwili wake umeungua vibaya,” alisema.
 
Baba wa mtoto huyo alisema kijana wake alikuwa akifanya biashara hiyo kwa lengo la kuanza elimu ya sekondari ya binafsi na kutokana na kuungua kwa duka hilo, amebaki hajui la kufanya, wakati hata gharama za matibabu hospitalini hapo zinamtesa.
Aliwaomba watu wote walioguswa na kuungua kwa mwanaye kumsaidia kwa kutumia namba zake za simu ambazo ni 0786 89 51 14 au 0754 67 62 39

SAKATA LA KUBWA WATOTO LATIKISA TENA JIJI LA DAR

Wanafunzi wa shule ya msingi wakitoka madarasani baada kutokea kwa hali ya vurugu.
Lile sakata la utekaji na upoteaji wa watoto ambao wengi ni wanafunzi wa shule za msingi katika Jiji la Dar na kudaiwa linafanywa na watu walio kwenye magari aina ya Toyota Noah limeingia katika sura nyingine.

Ijumaa, 3 Oktoba 2014

NSSF YADHAMINI NA KUSHIRIKI KONGAMANO LA CHAMA CHA MAAFISA RASLIMALI WATU

Meneja Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo akitoa mada wakati wa kongamano la HRSTA Panorama lililowashirikisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Rasilimali Watu kutoka taasisi mbalimbali lililofanyika kwenye Hotel ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.
Meneja Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo akitoa mada wakati wa kongamano la HRSTA Panorama lililowashirikisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Rasilimali Watu kutoka taasisi mbalimbali lililofanyika kwenye Hotel ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.

HAYA KAZI HIYOOOO KIJANA CHANGAMKIA

 
BBC Swahili ofisi ya Nairobi inamtafuta mwandishi habari mwenye uwezo wa kuripoti na kutangaza kwa lugha ya Kiswahili.
 
Pia lazima uwe na uzoefu wa maswala ya kidijitali.

Kwa maelezo zaidi kuhusu nafasi hii ya kazi bonyeza hapa: http://goo.gl/GUrD0h

KIONGOZI WA BOKO HARAM ASEMA HAJAFA

Kiongozi wa Boko Haram Abubakr Shekau
Kanda ya video inayomuonyesha mtu anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi la Boko Haram imetolewa akikana madai ya jeshi kwamba amefariki.
Katika kanda hiyo,Abubakr Shekau anasema kuwa wapiganaji wake waliitungua ndege ya wanajeshi wa angani iliotoweka wiki tatu zilizopita.
Wiki iliopita jeshi lilidai kuwa mtu anayejionyesha katika kanda ya video ya Boko Haram aliuawa na mwezi Agosti 2013 likadai kwamba huenda Shekue amefariki.
Wachanganuzi wametilia shaka kuhusu uthabiti wa madai hayo ya jeshi.
Wapiganaji wa Boko Haram
Mwandishi wa Nigeria Ahmad Salkida, ambaye ana mawasiliano mazuri na Boko Haram alisema kuwa katika mtandao wake wa Twitter wiki iliopita ana uhakika kwamba Shekue yu mzima buheri wa afya na kwamba hajafariki.
Haijabainika ni lini ama wapi kanda hiyo ilikopatikana na shirika la habari la AFP ilisema kuwa video hiyo ilitengenezwa.

Mhariri wa Idhaa ya BBC ya Hausa, Mansur Liman ,amesema kuwa mtu aliyezungumza katika kanda hiyo ya video alikuwa Abubakr Shekue yule yule anayeonekana katika kanda nyengine za video za kundi la Boko Haram.

WANAFUNZI 40 WAPOTEA NCHINI MEXICO

Mamia ya wanafunzi nchini Mexico katika jimbo la Guerrero wameandamana katika mji mkuu wa jimbo la Chilpancingo kulalamikia kutoweka kwa zaidi ya wanafunzi wenzao arobaini wiki iliyyopita.

Wanafunzi hao wanasemekana kuwa mwisho walionekana kusombwa katika magari ya polisi kufuatia maandamano walioshiriki wakilalamikia ubaguzi katika ajira ya walimu wa maeneo ya vijijini.

Polisi walifyatua rissasi kwenye basi na kwa waandamaji na kuua watu sita na wengine 17 kujeruhiwa.

Maafisa ishirini na wawili wa polisi wanashikiliwa na kwa kutuhuma za kuwafyatulia risasi wanafunzi hao.

Ndugu wa waliouawa wanaosaidiwa na polisi waliingia mlango kwa mlango katika eneo la Iguala wakiwa wameshikilia picha za wapendwa wao na kutafuta eneo ambalo miili ya ndugu zao ilipofichwa.

Serikali ya jimbo hilo imetoa dola 75,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa kueleza wanafunzi hao walipo.

PROFESA LIVIGHA ALIYEUAWA KWA RISASI AZIKWA DAR

Mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha ukiwasili nyumbani kwake Bunju jijini Dar leo.
Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala (wa pili kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe (wa tatu kushoto) msibani kwa Profesa Athuman.
Mwili wa Profesa Athuman ukiingizwa nyumbani kwake Bunju, Dar.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.
Mwili wa marehemu ukioswaliwa kabla ya maziko.
Mwili wa Profesa Athuman Livigha ukipelekwa makaburini kwa maziko.
Mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Athuman Livigha, aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake, Bunju jijini Dar es Salaam umezikwa leo.
Marehemu aliuawa Septemba 30, mwaka huu majira ya saa 3 usiku akiwa nyumbani kwake. (PICHA: MAKONGORO OGING' NA HARUNI SANCHAWA / GPL)

Alhamisi, 2 Oktoba 2014

SITTA AMSAMEHE MNYIKA


Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta.


MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta amelieleza Bunge hilo kuwa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), aliamua kumtukana yeye na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge.

“Bwana mmoja Mnyika ameamua kututukana mimi na Chenge…ametuita maharamia mbele ya mkutano wa hadhara huko Mwanza.

“Mimi kwake ni baba yake na kama hawezi kuniheshimu, basi aniheshimu kama mtu mzee katika nchi hii…lakini namsamehe kwa kuwa ni kijana mdogo, huenda ndio anakomaa kisiasa lakini sisi Watanzania tunatumia lugha yetu kwa staha,” alisema Sitta.

Alifafanua kuwa Mnyika ametoka chuoni juzi juzi na siasa anazoziendesha ni za kivyuo vyuo, ambazo alisema kama ndio zitakuwa siasa za chama hicho, itachukua muda kushika madaraka. Hata hivyo, alipokuwa akisema ametoka chuo kikuu juzi juzi, wajumbe walipiga kelele wakisema: “Hajamaliza chuo! hajamaliza chuo!”.

Vitisho vingine, Ukawa Mbali na waraka huo na Mnyika kufanya jitihada ili Katiba inayopendekezwa isipatikane, Sitta alisema baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walitishwa ili wapige kura ya Hapana na wamekiri mbele ya Katibu wa Bunge.

“Kuna wajumbe wawili wamekwenda kwa Katibu na kuonesha ujumbe wa simu wa maneno wa vitisho, wakitakiwa kuondoka hapa Dodoma, wametishwa sana kiasi tumewaruhusu waondoke.

“Mjumbe mwingine alifungiwa ndani jana (juzi) ili asije kupiga kura…kumfungia mtu ndani ni jinai sasa watu wanatuchukia mpaka wanafungia watu ndani? Ilibidi tuwasiliane na vyombo vya ulinzi na usalama ili afunguliwe na alipiga kura,” alisema Sitta.

Mbali na hao, Sitta alitoa taarifa kuwa kuna mjumbe ambaye jina lake lilimtoka, ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kushawishi wajumbe kutoka Zanzibar, na hasa wenye muelekeo wa kuunga mkono CUF, wapige kura ya ‘Hapana’.

Mmoja wa wajumbe ambaye alishawishiwa na mjumbe huyo na kushikilia kama ‘mfungwa’ kwa mujibu wa Sitta, ni Mwanaidi Othman Twahir, ambaye alipiga kura ya ‘Hapana’.

Hata hivyo, Sitta alisema Mwenyekiti wa chama chake cha NRA, alituma ujumbe kusema kuwa mjumbe huyo hana elimu kuhusu kinachoendelea, ndio maana alipiga kura ya ‘Hapana’ lakini yuko tayari kupiga kura upya.

Sitta alisema kutokana na rai hiyo ya Mwenyekiti wa NRA, aliruhusu kura hiyo irudiwe lakini baada ya kukamilika kwa kazi ya Kamati ya Mashauriano.

Pamoja na harakati za mjumbe huyo, Sitta alisema kuna baadhi ya wajumbe wawili waliotoka nje (kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi), baada ya kusoma Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, waliifurahia na kuona ni uzalendo kupiga kura. Hata hivyo, hakuwataja.HABARILEO