RAIS KIKWETE.
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, ameisifu Serikali ya Awamu ya Nne na kudai ndiyo iliyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kiwango kikubwa sana kuliko awamu nyingine zilizopita.
Lowassa aliyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara baada ya kuweka jike la msingi la ujenzi wa hospitali ya kisasa wilayani humo na kusisitiza kuwa, ujenzi huo ni matokeo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.RAIS KIKWETE NA EDWARD LOWASSA KUSHOTO.
"Ndugu zangu wana Monduli, huu ni uthibitisho wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama chenu, lazima niseme wazi kuwa, hakuna kipindi ambacho ilani hii imetekelezwa kwa kiwango kikubwa kama awamu hii chini ya Rais Jakaya Kikwete," alisema.
Hospitali hiyo ambayo majengo yake yatakamilika Februari 2014, ujenzi wake utagharimu zaidi ya sh. bilioni mbili ikiwa na uwezo wa kulazwa wagonjwa 72 katika wodi nne.
"Nilipotoa ahadi ya kujenga hospitali hii, nilizingatia ilani ya CCM hivyo chama chetu kinastahili pongezi na Rais Kikwete kwa kusimamia kidete ilani yetu ya uchaguzi," alisema.
Lowassa aliongeza kuwa, hospitali hiyo ikikamilika itakuwa na vifaa vya kisasa na kuifanya moja ya hospitali bora nchini.
Alisema alimfuata Rais Kikwete na kumuomba fedha kwa ajili ya mradi wa maji na kupewa sh. bilioni tatu ambazo ziko benki ambapo msaada huo umelenga kutimiza ilani ya CCM.
"Ndiyo maana nasema hakuna wamu ambayo imetekeleza ilani ya uchaguzi kwa asilimia kubwa kama awamu hii ya Rais Kikwete, pia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
"Mkataba huu ni wa ujenzi wa nyumba 100 na kati ya hizo, 50 zitapangishwa na nyingine za kuuza," alisema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni