Mwakilishi wa kampuni ya Delina Group (DGE) kushoto,Bw. Emmanuel Mzava,akionyesha waandishi wa habari vifaa vya michezo vilivyotolewa na Bw. Davis Mosha. Kulia ni Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media Group Bw. Alex Kassuwi (kulia).
Kampuni ya Delina Group (DGE) inayomilikiwa na Bw. Davis Mosha imekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya mamilioni ya pesa pamoja na vikombe kwa ajili ya kumtafuta Bingwa wa Uhuru Cup kwa timu za mpira ambazo zinaundwa na watanzania ambao wanaishi nchini Marekani na ni mashabiki wa Simba na Yanga. Tarehe za mechi hizo zitatajwa hivi karibuni tukishirikianana ubalozi wa Tanzania.
Mwakilishi wa kampuni ya Delina Group (DGE) kushoto,Bw. Emmanuel Mzava,akimkabizi vifaa vya michezo,mwakilishi wa mashabiki wa Simba na Yanga wanaoishi Marekani Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media Group Bw. Alex Kassuwi (kulia).
Aidha Emmanuel ameongeza kuwa,lengo la Kampuni ya Delina Group (DGE) kudhamini timu hizo zinazoundwa na mashabiki wa Simba na Yanga zilizopo ugenini,ni kuweka hamasa ya ushindani ndani na nje ya nchi,na kuongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu.
kutoka kushoto ni Emmanuel Mzava wa Delina Group (DGE) na kulia anayezungumza ni
Alex Kassuwi Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media Group wamiliki wa Swahili Radio Online, Swahili TV online, Swahilitv blog, na DMK411 blog
Alex Kassuwi Mkurugenzi wa Swahili Media International, MMK Media Group wamiliki wa Swahili Radio Online, Swahili TV online, Swahilitv blog, na DMK411 blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni