Ijumaa, 15 Novemba 2013

Ni hali ya kusikitisha Ufilipino

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufilipino, ameambia BBC kuwaidadi kamili ya watu waliojeruhiwa kutokana na Kimbunga Haiyan, wiki jana, imefika watu elfu tatu na mia tano.
Bwana Mar Roxas amekiri kuwa idadi hiyo hata hivyo huenda ni kubwa zaidi ya hiyo.

Ingawa idadi rasmi ya waliofariki bado haijulikani na maafisa katika moja ya majimbo yaliyoathirika zaidi kuliko yote, wanasema kuwa watu elfu nne wamefariki jimboni humo pekee.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa serikali italazimika sasa kuanza kufanya mipango ya ujenzi mpya na wa kudumu.
Serikali inakadiria uharibifu uliotokea kuwa wenye thamani ya dola bilioni 15.
Asilimia tisini ya nyumba zimeharibika na maelfu ya shule haziwezi tena kutumika.
Watoto hawaendi tena shule hadi mwezi Januari.2014.
Wakati huohuo, wafanyakazi wa kutoa misaada nchini wametaja hali iliyoko nchini humo kama ya kusikitisha, wiki moja tu baada ya kimbunga Haiyan kupiga maeneo ya kati ya nchi hiyo. Maelfu ya raia wa nchi hiyo bado wanahitaji misaada ya dharura.
Msemaji wa shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka, la Medicins sans Frontiers, Henry Gray, amesema masuala mengi ya mipango yanaathiri shughuli ya kusambaza misaada.
Katibu mkuu wa muungano wa nchi wanachama wa muungano wa asia na pacific ASEAN Lee lair-un min amesema misaada zaidi itatolewa na kuwa mataifa yote duniani yanaweza kufanya mengi zaidi kusaidia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni