Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba katika tamasha la Krismas lililofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki huo hapa nchini na mwimbaji wa kimataifa kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti wamesuuza mioyo ya mashabiki baada ya kushusha burudani ya nguvu katika tamasha hilo, Katika tamasha hilo, mashabiki wamejitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Jamhuri, Tamasha hilo linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam na linatarajiwa kuendelea mkoani Tanga Desemba 28 mwaka huu.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MOROGORO)
Mwimbaji Edson Mwasabwite akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo jioni.
Boniface Mwaiteje naye akawanyanyua kwenye viti mashabiki waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
Mwanamama mwenye sauti ya mirindimo Upendo Nkone akakonga nyoyo za mashabiki wake.(P.T)
Hapa akiimba kwa furaha kumtukuza mungu wake mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wa Jamhuri.
Vijana wa kazi kutoka kundi la Kitimtim la Rose Muhando wakionyesha umahiri wao katika kucheza.
Upendo Nkone akicheza na mastaeji shoo wake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni