APOTEZA MAISHA KWA TUHUMA ZA KUIBA KUKU WANNE TU HUKO SHINYANGA.
Kijana mmoja ameuawa na wanchi wenye hasira kali baada ya kumtuhumu kuiba kuku wanne. Polisi imemtaja kuwa ni Ngaga Shija ambaye alipewa kipigo na kisha mwili wake kuchomwa moto, alikuwa akituhumiwa kuiba kuku hao katika kijiji cha Ikonda.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evaresti Mangala, kabla ya kifo, Shija alikuwa nje kwa dhamana katika kesi iliyokuwa ikisikilizwa Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga, akikabiliwa na mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kupatikana na mali ya wizi.
Aliuawa juzi saa 2 asubuhi katika Kijiji cha Isagala Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu. Hata hivyo Kamanda alisema mmiliki wa kuku wanaodaiwa kuibwa, hajafahamika. Wananchi
wakimwadhibu kibaka baada ya kutumu kufanya mambo yanayopingana na jamii yenye
watu wastaraabu. Picha na Maktaba. KIJANA mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Kijiji cha
Isagala, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, ameuawa na watu waliojichukulia
sheria mkononi wakimtuhumu kuiba kuku wanne. Aidha katika tukio lingine wilayani Tarime mkoani Mara,
mtuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha , Senso Mwita ameuawa katika kile
kilichoelezwa ni kwenye majibizano ya kurushiana risasi na polisi.
Katika tukio hilo, mtuhumiwa huyo wa
ujambazi wa kutumia silaha , inadaiwa alikuwa na wenzake wawili ambao
walijibizana na polisi kwa kurushiana risasi.
Mwita anayekadiriwa na
umri wa miaka kati ya 25 na 30, inadaiwa alikuwa akisakwa na Polisi muda mrefu
kwa kuhusika na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha na mauaji katika Tarafa
ya Ingwe.
Kamanda wa Polisi Tarime / Rorya, Justus Kamugisha alisema
mwezi uliopita kulikuwa na matukio ya mauaji ya watu katika vijiji vya
Keisangura , Nyamwaga , Genkuru, Mriba na Nyarero.
Alisema usiku wa
kuamkia Januari 5, Polisi ilipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo na
kuonekana kundi la majambazi katika kitongoji cha Ntarechagini Kijiji cha
Nyamwaga.
“Wakati askari wetu wakiwa njiani kuelekea katika kitongoji
hicho, ghafla walishambuliwa kwa kurushiwa risasi na majambazi watatu na hapo
ndipo askari wetu walianza kujibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi mmoja wao kwa
jina la Senso Magabe Mwita,” alisema Kamanda.
Kwa mujibu wa Kamanda,
Mwita alikuwa na silaha aina ya SMG iliyofutwa namba zake na risasi 21. Wenzake
walitoroka na yeye alifariki kutokana na majeraha ya risasi akiwa njiani
kupelekwa hospitali ya wilaya.HABARILEO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni