Ijumaa, 31 Januari 2014

GARI DOGO AINA YA TOTOTA COROLLA T 379 AGL LAPATA AJALI WATATU WAJERUHIWA


Gari ndogo aina ya Toyota Corolla lenye nambari za Usajili T 379 AGL, likiwa ndani ya mtaro mara baada ya kupoteza mwelekeo wakati likiwa kwenye Mwendo mkali.
Tukio hili limetokea mchana huu katika Barabara ya Migombani kama unaelekea Makao Makuu ya Kampuni ya simu za Mikononi ya Zantel. Ndani ya Gari hii kulikuwa na watu watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika kwa haraka kutokana hali iliyokuwa, watu wawili kati yao wameumia vibaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
 Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa, gari hiyo ilionekana ikiwa kwenye mwendo kasi hali iliyopelekea kushindwa maarifa kwa dereva wakati akipishana na Bajaj.
Wasamaria wema wakihangaika namna ya kumuokoa mmoja wa majeruhi kwenye ajali hiyo, ambaye alikuwa amenasa kutokana na kubanwa na sehemu ya gari hilo.
Huu ndio mwonekano wa gari hiyo baada ya kuingia kwenye mtaro huo.
Mdau akionyesha kibao cha namba cha Gari hiyo ambacho kiling'oka na kuingia mtaroni.
Wasamalia wakiengelea kuhakikisha kama kuna mtu mwingine ndani ya Gari hiyo.
Majeruhi wakipakiwa kwenye Gari tayari kwa kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Gari iliyowapakia Majeruhi hao ikiondoka eneo la tukio. (TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni