Rais
Jakaya Kikwete amesema ili kuhakikisha sekta ya kilimo inapiga hatua lazima
ugunduzi wa teknolojia mpya zinazogunduliwa zitumike kwa vitendo. (HM)
Rais
Kikwete alisema bila kuviwezesha vituo vya utafiti na kuwatumia wataalamu wengi
wa kilimo kama mabwana na mabibishamba, sekta hiyo haitapiga hatua.
Alikuwa
akifungua mkutano wa wadau wa kilimo na biashara kutoka nchi mbalimbali za
Afrika na Ulaya, jana.
Alisema
uhifadhi wa vyakula katika maghala hauridhishi, kutokana na asilimia 30 ya
mazao yanayohifadhiwa huharibika jambo ambalo linaweza kuepukika likitafutiwa
ufumbuzi.
"Tunatakiwa
kutumia ugunduzi wa teknolojia mpya zinazogunduliwa ndani na nje ya nchi kwa
vitendo, ili kusaidia kuboresha kilimo nchini jambo ambalo linawezekana
tukiamua hasa kwa kushirikiana na wadau wengine," alisema Rais Kikwete.
Alisema
wakulima wengi hususan wadogo wanatakiwa kupewa elimu jinsi ya kulima mazao
ambayo yanaendana na udongo wa eneo husika, kazi ambayo inatakiwa kufanywa na
mabwana na mabibishamba na wadau wa kilimo.
"Pia,
rasilimali fedha na watu katika vituo vyetu vya utafiti wa kilimo vinahitaji
kuongezewa nguvu, ili kufanya tafiti nyingi na zitakazoweza kusaidia kutatua
matatizo," alisema.
yanayowakumba
wakulima wengi."
Awali
akimkaribisha Rais Kikwete, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher
Chiza alisema aliwataka washiriki wa mkutano huo kujadili jinsi ambavyo wataweza
kuwasaidia wakulima wadogo kuondokana na matatizo yanayowakumba kwa kutumia
gunduzi za kisasa zinazovumbuliwa. Chanzo: Mwananchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni