Alhamisi, 30 Januari 2014

SHILINGI ELFU KUMI ZAMTOA ROHO MFANYABIASHARA KENYA

Mfanyabiashara mmoja nchini Kenya amekutwa amekufa wilayani Nyamira kaskazni mwa Kenya..
Marehemu huyo James Keongo Ndubi, alisemekana kuwa ameenda kumdai mdeni wake sh 10,000 za Kenya sawa na sh 180,000 za Tanzania siku ya Jumanne lakini akaripotiwa kuwa hajulikani aliko siku hiyo hiyo.
Baada ya siku moja mwili wake ulionekana ukining'inia kwenye mti eneo la Boisanga.
Ndugu zake wanadai kuwa kuna mchezo mchafu umefanyika kwani alikuwa na majeraha kweny kichwa, miguuni na mikononi.
POST MORTEM
Taarifa kutoka kwa mpwa wa marehemu Bw Benard Momanyi, watafanya post mortem ili kubaini chanzo zha kifo hicho.
Mkuu wa Police huko Nyamira Shadrack Maithyaamethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa:
“Mwanzoni tulichukulia kifo hicho kuwa ni cha kujinyonga lakini baada ya hizi taarifa mpya tutafanya uchunguzi wa kina.”
Aliwaomba wananchi wenye taarifa zozote waisaidie polisi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni