Jumatano, 26 Machi 2014

BREAKING NEWS: MVUTANO MKALI BUNGENI BUNGE LAAHIRISHWA

sita
Bunge Maalum la Katika limekutana   leo jioni hii kuendelea na shuguli zake Lakini mvutano mkubwa umejitokeza hali iliyosababisha vurugu kubwa Iliyoambatana na zomea zomea. Mvutanho huo uliibuka  pale mjumbe wa Bunge hilo Mhe. Tundu Lissu aliposimama kuomba muongozo Kuhusu Marekebisho ya Kanuni kmbayo Tundu Lissu anamtuhumu Mwenyekiti wa Bunge Hilo kupitia Kamati ya Uongozi kuleta Marekebisho Kinyume cha kanuni zilizopitishwa na bunge hilo la Katiba.
 
Mwenyekiti wa Bunge Hilo Mh Samwel Sitta aliingilia kati kujaribu kutoa ufafanuzi  pamoja na wajumbe wengine akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali lakini hali ya zomea zomea iliendelea ndipo mwenyekiti wa Bunge hilo alipolazimika kuliahirisha Bunge hilo mpaka kesho na kuamuru mabadiliko hayo yapelekwe kwenye Kamati ya Kanuni

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni