Pichani: Hafidhi kabla na baada ya kutumia Metakelfin
Hafidh Masokola mwenye umri wa miaka 47, mkaazi wa Tabora amedai kuwa alitumia dawa aina ya Metakelfin miaka minne iliyopita kwa lengo la kutibu ugonjwa wa malaria, lakini dawa hizo zilimsababishia madhara makubwa katika ngozi yake na kumpelekea kuwa albino.
Akiongea na Sun Rise ya 100.5 Times Fm, Hafidh ambaye ni mjasiriamali ameeleza kuwa alinunua dawa hizo ‘Pharmacy’ na kwamba baada ya kumsababishia madhara hayo ameamua kujiunga na chama cha maalbino Tanzania kwa kuwa anafanana na albino wengine.
Ameeleza kuwa katika hatua za awali za dalili mbaya ya ngozi yake, alimuona daktari wa ngozi wa mkoa wa Tabora na alipewa ushauri ambao hata hivyo baada ya kuufanyika kazi hali iliendelea kuwa mbaya.
Ameeleza kuwa katika hatua za awali za dalili mbaya ya ngozi yake, alimuona daktari wa ngozi wa mkoa wa Tabora na alipewa ushauri ambao hata hivyo baada ya kuufanyika kazi hali iliendelea kuwa mbaya.
“Ikabidi nikamuone daktari wa ngozi wa mkoa wa Tabora, anaitwa Dr. George. Nikaenda nikamuonesha zile dalili, akaniambia hii itakuwa tube za hydrocotzone baadae itapotea hiyo, basi mimi nikatumia zile tube za hydrocotzone, lakini ikawa hainisaidii kitu. Matokeo yake yale malengelenge yakahamia kwenye mguu, juu ya unyayo lakini yalikuwa hayana dalili zozote za muwasho….” Ameeleza.
“Nikaanza utaratibu wa kupakaa mafuta ya Vaseline muda kama wa wiki mbili hivi, lakini kikawa naona kama nikipakaa kwenye viganja…lakini hayaoneshi kama mafuta unapakaa, yanazama moja kwa moja kwenye ngozi. Ukipakaa kama dakika moja hivi ukipakaa unaona kama hujapakaa…” Hafidhi amesema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni