Jumatatu, 31 Machi 2014

LIVERPOOL YAIADHIBU SPURS KWA BAO 4-0 NA KUSHIKILIA USUKANI BAADA YA KUISHUSHA CHELSEA WA LIGI KUU ENGLAND


Suarez akifunga bao lake la 29 katika ligi kwa msimu huu wakiizamisha Spurs kwa 4-0

VIJOGOO wa Anfield, Liverpool imekwea hadi kileleni mwa Ligi Kuu ya England wakiiporomosha Chelsea baada ya kuifumua bila huruma Tottenham Hotspur iliwatembelea kwenye uwanja wao.


Liverpool iliitambia vijogoo wenzao wa London kwa kuwakandika mabao 4-0, na kuwafanya wafikishe jumla ya pointi 71, mbili zaidi ya Chelsea ambao jana walifumuliwa bao 1-0 na Crystal Palace.


Wageni walianza kujitabiria janga baada ya Younes Kaboul kujifunga dakika ya pili ya mchezo kabla ya Luis Suarez kuandika bao la pili dakika ya 25 na wenhyeji kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 2-0.


Kipindi cha pili kilianza kwa Liverpool kuandika bao la tatu kupitia kwa Phillipe Countinho dakika ya 55 kabla ya Jordan Henderson katika dakika ya 75 na kuifanya Liverpool kukalia kiti cha uongozi kilaini (TK).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni