Ijumaa, 21 Machi 2014

MARUFUKU KUMPA MTOTO MAJINA HAYA SAUDIA

Screen Shot 2014-03-21 at 5.23.39 AM.

Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imepiga marufuku majina hamsini ambayo yapo kinyume na tamaduni pamoja na dini ambapo kuanzia sasa, wazazi kutoka falme hiyo hawataruhusiwa tena kuwapa watoto wao.


Majina hayo ni kama Linda, Alice, Elaine au Binyamin (jina lenye maana Benjamin) ambapo jina la Benjamin (Binyamin) kwa dini ya kiislamu linaaminika kuwa jina la mtoto wa mtume Jacob, yaani Yacoub kwa dini.

Mengine katika orodha hiyo ambayo hayatoruhusiwa ni kwa sababu yanaaminika kuwa yenye kufuru, yasiyo ya kiarabu na yasio ya kiislamu au yenye kupingana na tamaduni na dini ya falme hiyo.

Sababu nyingine ni ya kigeni ama ya ughaibuni yakiwemo yenye maana ya ufalme au ukubwa, cheo fulani kama Sumuw (mtukufu), Malek (mfalme) na Malika (Malkia).

Screen Shot 2014-03-21 at 5.23.23 AMMajina mengine hayapo katika jamii hizi hivyo hakuna sababu zilizotolewa juu yake, hii ni sehemu nyingine ya orodha yenyewe ambapo ni Malaak (angel), Abdul Aati, Abdul Naser, Abdul Musleh, Binyamin (Arabic for Benjamin) Naris, Yara, Sitav.

Mengine ni Loland, Tilaj, Barrah, Abdul Nabi, Abdul Rasool, Sumuw (highness), Al Mamlaka (the kingdom), Malika (queen), Mamlaka (kingdom), Tabarak (blessed), Nardeen, Sandy, Rama (Hindu god), Maline, Elaine, Inar, Maliktina
Maya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni