Ndugu wa abiria waliosafiri na ndege ya Malaysia iliyopotea tarehe 8/3/2014 wametumiwa meseji (SMS) kuwa hakuna uwezekano wa kuwapata wakiwa hai abiria wote pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo.
Picha mpya za Satelilite zinaonesha kuwa ndege hiyo ilianguka katika sehemu moja ya bahari ya Hindi ikiwa na abiria 239.
Ujumbe wa simu ulisema: “Tunatakiwa kukubali kuwa ndege MH370 imepotea na hakuna abiria aliyepo hai.”
Binti wa Mmalaysia Andrew Nari, ambaye ni shabiki wa Liverpool na mhudumu mkuu wa ndege hiyo aitwaye Maira Nari aliandika ujumbe wa twitter: “Mungu anakupenda zaidi baba ... Mungu anawapenda nyie wote.” “Sijui cha kusema wala cha kufikiri, najiona nimepotea na nimechoka Usiku mwema Baba”
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni