Jumanne, 22 Aprili 2014

AUAWA KWA KISU NA MWANAMKE ALIYETAKA KUMBAKA

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina Stephen Philbert(30) mkazi wa Ngokolo mjini Shinyanga ameuawa kwa kuchomwa kisu wakati akifanya jaribio la kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 katika eneo la Ngokolo mjini Shinyanga usiku wa mkesha wa pasaka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla amesema kuwa tukio hilo limetokea Aprili 20, mwaka huu saa tisa usiku.
Amesema siku ya tukio mwanamme huyo alivunja dirisha la nyumba ya mwanamke huyo na kuingia ndani kisha kufanya jaribio la kumbaka lakini katika kujihami kwake ndipo mwanamke huyo alimchoma kisu kichwani ,akafariki dunia akiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi (TK).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni