Jumanne, 27 Mei 2014
MBUNGE WA NKASI ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI
Mbunge wa Nkasi mh. Ally Kessy asema Wazanzibar Wanachosha, ni Mzigo.
Kutokana na mjadala wa bajeti ya wizara ya mambo ya nje uliokuwa unaendelea , Mbunge wa Nkasi Ndugu Ali Kessy ameporomosha matusi mazito kwa wazanzibar kuwa ni watu wa hovyo na ambao kila mara wanalialia tu kuwa wanabaguliwa, wanadai mambo mengi kuliko uwezo wao na wakati hawachangii hata senti kwenye Muungano na hivyo kama wanaona wanaonewa waende kwenye nchi yao sio kukaa kwetu.
Alienda mbali zaidi kusema kuwa Zanzibar Majimbo ya uchaguzi ni madogo kiasi kwamba ukipigania filimbi wananchi wote wanakusanyika ila bado wanapewa fedha za mfuko wa Jimbo jambo ambalo sio haki, na pia hata umeme hawalipi na maji pia .
Jambo hili lilimfanya mbunge wa CCM ndugu Chombo, kuomba muongozo na Kumtaka naibu Spika amwambie Mhe Kessy kamwe asikanyage Zanzibar, hii ilikuwa baada ya kumuita mwendawazimu, na alisema ni bahati mbaya kwa CCM kuwa na mbunge mwendawazimu kama huyu.
Mbunge huyu alilalamika kuwa "Naibu Spika Mhe. Ndugai muda muda wote alikuwa akicheka, sijui nini maana yake"
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni