Bwana Juma ni Dereva Taxi maeneo ya Mwanyamala kwa Kopa
siku moja alifuatwa na jamaa mmoja ampeleke sinza kwenye nyumba Fulani ya wageni
.
Walipokaribia pale
Yule jamaa akasema ameishiwa chaji kwenye simu yake akamuomba juma simu yake
atumie kupiga ili awasiliane na mwenyeji wake pale nyumba ya wageni, simu ya
juma haikuwa na hela .
Walipokaribia ile nyumba ya wageni Yule jamaa
akaomba kushuka anunue vocha atie kwenye simu ya Juma ili awasiliane na mwenyeji
wake, Juma akakubali, jamaa akanunua vocha akaitia kwenye simu ya Juma halafu
akawasiliana na mwenyeji wake .
Walipofika sehemu husika jamaa akashuka
akaingia ndani ya nyumba kumfuata mwenyeji wake ambaye alikuwa mwanamke huku Juma
akiwa ameshaondoka zake kwa sababu alikuwa ameshakamilisha shughuli yake
.
Siku iliyofuata iligundulika maiti ya mwanamke ndani ya kile chumba,
simu ilikuwa mezani na vitu vingine vyote hakukuonesha kama kulikuwa na vurugu
au mikikimikiki yoyote ile.
Uchunguzi wa awali ulifanyika pale chumbani kwenye
kifaa cha kuwekea taka na simu ya yule mwanamke, hapo mwili wake ulikuwa chumba
cha maiti ukifanyiwa uchunguzi pia.
Kwenye kifaa cha kuwekea taka iligundulika vocha
moja iliyotumika, ilipofuatiliwa iligundulika iliwekwa kwenye simu ya Juma yule
dereva taxi na ikatumiwa kumpigia huyu mwanamke aliyekutwa na
mauti.
Dereva wa taxi akatafutwa akapatikana, kukaguliwa gari yake
ikagundulika vocha ingine ya simu iliyotumika katika moja ya milango ya taxi
hiyo .
Bwana Juma yuko ndani kwa mashtaka ya mauaji na uchunguzi
unaendelea kufanyika mpaka hapo itakapokuja kudhihirika kuwa si yeye aliyefanya
tukio hilo.
Inawezekana wewe ukawa ni bwana Juma ajaye, unayependa
kugawa simu yako tu kwa watu wapige, watu waingize vocha zao, watu waandike
ujumbe mfupi au wafanyie chochote kile bila kujua unachofanya kinaweza
kuhatarisha maisha ya wengine na yako pia.
Simu na namba yako ni mali yako imesajiliwa kwa
jina lako, wakati unasajili uliingia mkataba wa kutumia kifaa hicho bila
kuvunja sheria zozote za nchi muda wote .
Kina Juma wako wengi, tazama usiwe mmoja wao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni