Jumatano, 28 Mei 2014

MSAADA MSAADA MSAADA! KUMUOKOA MWAMKE WA SUDAN ALIYEHUKUMIWA KIFO

140527142840 mama sudan 512x288 bbc nocredit 9905b
Mwanamama Meriam siku ya harusi yake
Mwanamke aliyeasi dini nchini Sudan na kupata adhabu ya kifo amejifungua mtoto mvulana akiwa jela mjini Khartoum kwa mujibu wa wakili wake.
Meriam Yehya Ibrahim Ishag, aliolewa na mwanamume mkristo jambo lililopelekea mwanamke huyo kuhukumiwa kifo mapema mwezi huu baada ya kukataa kusilimu tena.
Ataruhusiwa kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu kutekelezwa.
Meriam aliyezaliwa na baba muislam na mama mkristo, alihukumiwa na mahakama ya ya kiislam.
Bi Ibrahim alihukumiwa kifo kwa kosa la zinaa kwa sababu ameolewa na mwanamume mkristo wa kutoka Sudan Kusini na kwamba ndoa yao haikubaliki chini ya sheria ya kiislam ambayo inasema kuwa mwanamke muislam hawezi kuolewa na mwanamume mkristo.
Kwa kosa hilo, jaji alimhukumu adhabu ya mijeledi mia moja, adhabu ambayo itatekelezwa pindi mama huyo atakapopata nafuu kutokana na kujifungua.
Bi Ibrahim alilelewa kwa njia ya kikristo, dini ya mamake kwa sababu babake aliyekuwa muislam hakuwepo katika maisha yake tangu utotoni.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International, alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Zinaa mwezi Agosti mwaka 2013, na mahakama ikamuongezea kosa la kuasi dini Februari 2014 aliposema kuwa yeye ni mkristo wala sio muislamu.
Sudan ina idadi kubwa ya waislam ambao wanafuata sheria za kiisilamu.
JAMII YA KIMATAIFA INAOMBWA LUSAIDIA KUMUOKOA MAMA HUYU AMBAYE KIMSINGI ANASTAHILI KUISHI. INGEFAA KAMA MTU ANGEANZISHA PETITION AMBAYO WAPENDA AMANI WATAWEZA KUSAINI ILI KUSAIDIA KATIKA HILI. (TK)
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni