Oduor alisema kuwa mkewe alimsaliti katika ndoa yao baada ya siku 13 ya harusi yao iliyofanyika wiki ya pasaka ambapo alimfumania mkewe akishiriki tendo la ndoa na mwanaume mwingine ikiwa ni siku 13 tu baada ya harusi yao kwa kumkuta moja ya hoteli jijini Nairobi Kenya.
Wawili hao walikua wakirejea nyumbani baada ya honeymoon ya siku tano pamoja katika jiji la kifahari la Malindi pwani ya Kenya ambapo harusi yao ya kufana ilifungwa kwenye kanisa la Pentecostal Assemblies of God Diani Mombasa.
Oduor amedai harusi yake ilikua ni ya kupoteza muda na pesa na ameapa kutoishi tena na mwanamke huyo na kujihusisha na uhusino wa kimapenzi tena kwani hana imani tena na Wanawake.
Kuachana kwao pia kulifanyika kwa kasi baada ya kugundua kwamba Sarah alikua amesambaza picha zake za uchi kupitia WhatsApp.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni