Jumatatu, 2 Juni 2014

U15 WAREJEA KIFUA MBELE

U15 TANZANIA YATUA MEDALI VIFUANI
Timu ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 15 iliyoshika nafasi ya pili katika Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) iliyofanyika Gaborone, Botswana inawasili leo (Juni 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
U15 ambayo imeshinda mechi tatu, sare moja na kufungwa moja inawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Gaborone kupitia Nairobi.
Tanzania ambayo imepata medali za fedha kwa kushika nafasi hiyo ikiwa chini yaKocha Abel Mtweve ilizifunga Afrika Kusini 2-0, Botswana 2-0, Swaziland 3-0 na ikatoka sare ya bao 1-1 na Mali. Ilifungwa mabao 2-0 na Nigeria ambao ndiyo walioibuka mabingwa.
Wachezaji 16 waliounda kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Ulomi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni