Mshambulizi wa Uholanzi Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya
timu yake ikapewa penalti ya ushindi lakini akasema alikuwa ametegwa .
Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemkashifu refarii wa mechi yao na Uholanzi
Pedro Proenca kwa kuipendelea Uholanzi .Robben alikfanyiwa faulu katika eneo la lango Uholanzi ilipokuwa imesawazisha bao moja kwa moja na ikaisaidia Uholanzi kuibuka mshindi kwa mabao 2-1 .
Penalti hiyo ilifungwa na Jan-Klaas Huntelaar
''Nafikiri kuwa refarii Proenca alifanya kweli kuashiria penalti akisema kuwa alikuwa ametegwa na nahodha wa Mexico Rafael Marquez.
Mexico ilikuwa imeongoza hadi dakika ya 88 ya kipindi cha pili kabla Wesley Sneijder kuisawazishia Uholanzi kabla ya Huntelaar kufunga penalti iliyozua ubishi mkubwa.
Herrera alisema kuwa haikufaa refarii kutoka ulaya alipewa mechi kati ya timu kutoka ulaya na Marekani ya kusini.
Kwanini FIFA hawakutupa refarii mwafrika mhindi ama hata refarii kutoka Marekani kusini ?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni