Hakuna njia ya kupita: Tim Howard akimnyima mchezaji mwenzake wa Everton ambaye anaichezea Ubelgiji, Kevin Mirallas kufunga bao kipindi cha pili.
MAREKANI imetupwa nje ya kombe la dunia baada ya kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wa 16, lakini mlinda mlango wako, Tim Howard ameweka rekodi mpya ya kombe hilo baada ya kuokoa michomo ya hatari 15.
Howard ndiye aliwapeleka wapinzani wao, Ubelgiji, kufika dakika 30 za nyongeza baada ya dakika tisini kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana, lakini katika dakika hizo, Howard alikuwa shujaa kwa kuokoa michono mingi golini kwako.
Kijana wa kazi: Howard aliokoa michomo mingi zaidi ukilinganisha na kipa mwenzake wa Ubelgiji, Thibaut Courtois
Howard akijitanua na kuokoa mpira uliopigwa na nahodha wa Ubelgiji Vincent Kompany
Kwa kuokoa michomo 15, kipa huyo wa Everton ameandika rekodi mpya ya kombe la dunia tangu takwimu kama hizo zipatikane mwaka 1966 ambapo kipa wa Peru, Ramon Quiroga aliokoa michomo 13 mwaka 1978 dhidi ya Uholanzi.
Kiwango cha jana cha Howard ndio bora zaidi kuwahi kutokea katika timu ya Marekani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni