MIILI YA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA NDEGE YA MALAYSIA YAPELEKWA UHOLANZI
Mabaki ya ndege ya Malaysia yakiwa yamezagaa
Kwa mara ya kwanza miili iliyopatikana kutoka kwenye ndege ya
Malaysia iliyotunguliwa juma lililopita nchini Ukraine itasafirishwa mpaka
nchini Uholanzi kwa ajili ya kutambuliwa.
Uholanzi iko kwenye siku ya maombolezo kwa ajili ya watu 298 waliokufa kwenye
ajali hiyo, 193 kati yao raia wa Uholanzi.
Maafisa wa kiintelijensia wa nchini Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono
Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu
tukio hilo, vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.
Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka
na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.
Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi
chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni