Jumatatu, 11 Agosti 2014

MTU MMOJA AUAWA MJINI MOROGORO NA KUCHOMWA MOTO

Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja ameuawa kikatili kisha mwili wake kuchomwa moto na watu wasiofahamika katika eneo la mkundi manispa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa wananchi walishuhudia tukio hilo wamesema wameshuhudia kundi la madereva wa pikipiki wakimshusha mtu huyo kisha kummwagia mafuta ya taa na kumchoma moto ambapo wameomba jeshi la polisi kufuatilia tukio hilo walohusika wachukuliwe hatua.

Wananchi wakazi wa kata ya Mkundi wamesema hilo sio tukio la kwanza kutokea kwa watu kuuawa na kisha kuchomwa moto na kuomba vyombO vya sheria kufanya kazi zake kwani huenda matukio hayo yanatokana na watu kuchoshwa na baadhi ya matukio ya wizi ambayo watuhumiwa huachiwa huru na vyombo vya sheria pasipo kuchukuliwa hatua.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni