Mwili wa Joseph Gabriel ukiwa barabarani kusubiri jeshi la polisi waje kuuondoa
Kijana Joseph Gabriel anayefanya vibarua mbalimbali vya kujiingizia
kipato amekutwa amekufa baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na
huku sehemu ya pua ikiwa imeondolewa sambamba na sehemu ya shavu lake la
kushoto.Mauaji haya ya
kutisha yametokea katika maeneo ya kata Karabagaine katika kijiji cha
Kitwe.Polisi pia walichelewa kufika eneo la tukio kutokana na kuwa
katika eneo jingine ambako pia kulikuwa na tukio jingine la kutisha kama
hili lilitokea siku moja kabla ya hili.Mwanamke mmoja
ambaye jina halikuweza kufahamika mara moja, amekutwa amekufa kwa
kuchinjwa shingo na pua yake kuondolewa.Pua yake ilipatikana baadae
karibu na eneo la tukio.Mama huyu amekutwa na mauti katika mtaa wa
Kibeta kata ya Kibeta ambapo baadaye polisi waliweza kufika na kuchukua
mwili wa marehemu.
Mabaki ya damu baada ya mwili wa mwanamke kuondolewa na polisi
Mwezi
uliopita, polisi Kagera ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu
mauaji ya manispaa ya Bukoba, ikieleza kuwashikilia watu kadhaa na
kinara wa mauaji hayo, ambao majina yamehifadhiwa kwasababu za
kiusalama, huku ikisema kuwa watu wawili waliuawa na polisi kwa kupigwa
risasi, wakati wakiwapeleka kwenye maeneo wanakopangia uhalifu huko
Bugabo halmashauri ya Bukoba.
My Take:
Imefikia muda sasa wakazi wa Manispaa ya Bukoba tunasema inatosha.Mji
umekosa amani pia vyombo vyenye mamlaka havifanyi jitihada kubwa kuzuia
mauaji haya.
Ndugu wanaJF, ni kwamba haya mauji sasa yamekuwa shida kwa muda mrefu,watu hatuna amani maana hujui kama siku utaimaliza salama.
Nimemuuliza Mbunge wa Mh. Kagasheki kwenye "JF's Exclusive Interview" ila kwa bahati mbaya sijapata majibu.
Mkuu wa
polisi Kagera,Bukoba sijui wanatuhakikishiaje usalama wetu au ndio
wanataka wananchi wenye hasira kali wachukue sheria mkononi.
#MauajiBukobaYatosha
CHANZO ; JAMII FORUM
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni