Jumatano, 27 Mei 2015

SEVILLA YAHIFADHI KOMBE LA UEFA

Fainali kati ya Sevilla dhidi ya Dnipropetrovsk
Usiku wa kuamkia leo kulikuwa na kivumbi cha fainali ya Uefa ndogo, kwenye mtanange ulioikutanisha Sevilla ya Hispania dhidi ya Dnipropetrovsk ya Ukrain.

Katika mchezo huo uliopigwa mjini Warsaw nchini Poland, Sevilla imeibuka kidedea kwa jumla ya bao 3-2, huku shukrani za dhati zikienda mkolombia Carlos Bacca aliyetumbukiza kimiani mabao mawili kati ya matatu yaliyoipa ushindi Sevilla.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa timu hiyo kunyakua kombe hilo na kuweka rekodi ya kuchukua mara nyingi zaidi taji hilo. Ukiachilia mbali ushindi huu walioupata jana, Sevilla ilitawazwa kuwa mabingwa kwa mara ya kwanza mwaka 2006, 2007 na 2014.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni