Jumanne, 12 Agosti 2014

WIVU WA MAPENZI WAZUA BALAA


Shao Zongqi akiwa mahakamani
Waswahili husema wivu ni kidonda ukiushiriki utakonda. Kauli hii inakuja baada ya mwanamume mmoja kuua watu 6 baada ya mkewe kujihusisha na wanaume hao kingono, kutokana na tukio hilo mwanamume huyo amehukumiwa adhabu ya kifo nchini China.
Shao Zongqi, mwenye umri wa miaka 38 alikutwa na hatia baada ya kutekeleza mauaji hayo mwezi January mwaka huu, alipoua katika mji wa Yunnan.
Kwa muujibu wa mahakama, Shao alipanga kulipiza kisasi baada ya kugundua kuwa mkewe alikuwa na mahusiano na wanaume wawili tofauti, shirika la habari la Xinhua limeeleza hayo.
Wakati wa sherehe za mwaka mpya wa kichina, Shao alijeruhi wanaume tisa, na kumuua mmoja pamoja na familia yake na wanaume wengine wawili wa jirani, wakati mwanamume mmoja akiwa na mkewe na mtoto wao wa kiume walinusurika katika tukio hilo.
Wakati hukumu hiyo ikitolewa siku ya jumatatu, iliamuriwa Shao alipe kiasi cha yuani 604,000/- sawa na dola za kimarekani 98,000/- kwa familia walio hai ambao waliondokewa na jamaa zao kutokana na shambulio hilo.Pamoja na kulipa faini hiyo Shao ameapa kukata rufaa kutokana na hukumu hiyo ya kifo inayomkabili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni