Pikipiki aina ya Suzuki ikiwa imenasa mbele ya Lori baada ya kugongana uso kwa uso .Ajali imetokea barabara kuu ya Arusha Moshi ikihusisha Lori aina ya Scania lenye namba za Usajili T 137 ATA na pikipiki aina ya Suzuki yenye namba SU 40262 mali ya Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Katika ajali hiyo mwendesha pikipiki aliyefahamika kwa jina la George Lyamuya, mfanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi, alifariki dunia papo hapo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni