Ifuatayo ni kauli ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa Bumbuli Tanga kuhusu Naibu waziri ambae pia ni mbunge wa Bumbuli January Makamba.
Amenukuliwa akisema
‘January anafanya kazi nzuri ya ubunge pia ananisaidia sana kwa kazi ya wizara niliyompa, unajua January alipogombea Ubunge alinificha nilikuwa nasikia kwa wenzake tu pale ofisini, baadae alivyoweka mambo yake sawa ndio akaja kuniambia kwamba Mzee na Mimi najitosa’
‘Nikamtakia heri… kwa kweli kwa jinsi anavyohangaika na Jimbo lake inaonyesha Ubunge aliutaka kwa dhati kabisa ya kusaidia watu wa Bumbuli, nimesikia anafikiria mambo makubwa… hajaniambia mi nimesikia tu, namtakia kila la heri…. haya mambo anaamua Mungu wala hayalazimishwi’
‘Mungu akitaka linakuwa hata kama watu wote hawataki, Mungu akiwa hataki hata kama mtu ukitaka jambo hilo vipi haliwezi kuwa, mimi nilishauriwa na Mzee mmoja kwamba jambo likifika wakati wake utalipata hata kama utapingwa kiasi gani, kama halijafika wakati wake haliwezi kutokea, mimi niligombea 1995 sikupata kwasababu haikuwa wakati wake…. 2005 ikawa wakati wake nikapata, na wewe usipopata sasa usiweke nongwa” – JK
Hapa chini kuna video ya dakika 3 ikionyesha sehemu ya kazi zake Naibu waziri huyu ambae pia ni Mbunge wa Bumbuli kupitia CCM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni