Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa anaamini sheria inayowazuia makasisi katika kanisa hilo kuoa huenda ikaondolewa kulingana na wakati.
Katika mahojiano na gazeti la kitaliano la Republica, Papa Francis pia ameifananisha na ugonjwa wa ukoma hatua ya makasisi kuwanyanyasa kimapenzi watoto wadogo.
Amesema kuwa takriban asilimia mbili ya viongozi hao wa dini ikiwemo maaskofu pamoja na makadinali huwanyanyasa watoto kimapenzi,na kwamba yuko tayari kukabiliana na tatizo hilo kwa hali na mali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni