Habari kutoka Msumbiji zinasema serikali ya nchi hiyo
imetiliana saini na chama cha upinzani cha Renamo ili kumaliza uhasama kuelekea
uchaguzi wa mwezi Oktoba.
Mkataba huo unafuatia unafuatia mapigano ya chini kwa chini kati ya wafuasi
wa Renamo wenye silaha na majeshi ya serikali. Mwezi Oktoba mwaka jana Renamo
walijitoa katika mkataba wa amani uliotiwa saini kwa zaidi ya miongo miwili
iliyopita, mkataba ambao ulimaliza vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe.
Wiki iliyopita ikiwa sehemu ya makubaliano, serikali ya Msumbiji ilianza
kuwaachilia wafungwa wa Renamo waliokuwa wamekamatwa katika mapigano ya hivi
karibuni.
Tangu Msumbiji ijipatie uhuru wake tarehe 25 Juni 1975 kutoka kwa wakoloni wa
Kireno imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na waliokuwa waasi wa
renamo na sasa ni chama cha siasa cha upinzani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni