Gari aina ya Toyota Landcruiser VX lenye namba za usajili T540 APN lililopinduka maeneo ya Tazara.Polisi akilitazama gari lililopata ajali eneo la tukio.Pichani juu na chini Wananchi wakishuhudia kwa karibu zaidi ajali mbaya iliyotokea maeneo ya Tazara.
Ajali ya gari imetokea jana majira ya saa 10 za jioni katika maeneo ya Tazara jijini Dar es salaam. Dereva wa gari hili (Toyota Landcruiser VX lenye namba za usajili T540 APN) aliruka mapema kabla ya tukio kutokea na alikuwa peke yake. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba, dereva alipoteza muelekeo katika kulikwepa lori aina ya fuso lililokuwa kando ya barabara. Hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni