India imewakilisha 'Mangalyaan katika sayari ya Mars
Wanasayansi wa anga za juu nchini India wanasema kuwa chombo chao
cha safari za anga za juu kwa sasa kinazunguka sayari ya Mars.
Hii ndiyo mara ya kwanza kwa
India kutuma mtambo wake kwenda kwa sayari hiyo, safari ambayo imepata umaarufu
kutokana na gharama yake ya chini kabisa ya dola milioni 75 pekee.
India
ndilo taifa la nne duniani kufaulu kufikisha chombo katika sayari ya
Mars.
Mataifa mengine ambayo yamewasilisha vyombo vya utafiti wa anga za
juu katika sayari hiyo ni Marekani, Urusi na muungano wa mataifa ya
Ulaya.
kwa mahitaji ya kununua gari lililotumika kutoka Japan kwa bei nzuri
Chombo hicho ''The Mangalyaan robotic probe'' kinatarajiwa kuanza
upekuzi na uchunguzi wa hali ya anga katika sayari hiyo nyekundu.
Waziri
Mkuu nchini India Narendra Modi ambaye alishuduia mafaniko ya chombo hicho
kilichoanza safari yake miezi kumi iliyopita aliwapongeza wanasayansi hao kwa
ufanisi huo mkubwa. Roketi ya India 'Mangalyaan iliyotua katika sayari ya Mars
Aliwaambia kuwa mafanikio ya safari za anga za juu nchini India ni mfano
mwema wa hatua ambazo taifa hilo linaweza kupiga akisema kuwa ana mpango wa
kuboresha kitengo hicho.
Shirikisho la anga za mbali la Marekani NASA
ambalo lilifikisha chombo chake ''Maven'' katika sayari ya Mars Jumatatu wiki
hii, liliwapongeza wanasayansi wa India kwa ufanisi wao.
Kupitia kwa
ujumbe wa mtandao wa Twitter NASA iliandika kuwa ''Tunawapongeza @ISRO kwa
kuwasili katika sayari ya Mars. Mtajiunga na @MarsOrbiter kutathmini hali ilivyo
katika sayari hiyo. BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni