Ijumaa, 19 Septemba 2014

MATEKA WA 49 UTURUKI WAACHIWA HURU

Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu

Waziri mkuu nchini Uturuki amesema kuwa mateka 49 wa taifa hilo ambao walikuwa wametekwa na kundi la Islamic State kaskazini mwa Iraq wameachiliwa huru.

Ahmet Davutoglu amesema kuwa, mateka hao wakiwemo wanadiplomasia,wanajeshi na watoto walirudishwa hadi mji wa kusini wa Uturuki, Sanliurfa na maafisa wa ujasusi nchini humo.

Mateka hao walitekwa na wapiganaji hao katika shambulizi la ubalozi wa Uturuki katika mji wa Mosul mnamo mwezi Juni.

Uturuki imekuwa ikisitasita katika kuunga mkono Marekani kutekeleza mashmbulizi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State kutokana na usalama wa mateka hao.

Mnamo mwezi July madereva 32 wa malori kutoka Uturuki waliotekwa nyara katika tukio tofauti waliwachiliwa huru baada ya kuwa mateka kwa wiki tatu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni