Jumatano, 3 Septemba 2014

MWIZI WA NYAYA ZA TTCL APEWA MVUA NNE

Mmoja wa watuhumiwa wa nyaya za simu. Picha hii haina uhusiano na habari hii.
Mmoja wa watuhumiwa wa nyaya za simu. Picha hii haina uhusiano na habari hii.
Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam imemuhukumu kwenda jela miaka minne, Shaibu Muhidin Ndina baada ya kupatikana na kosa la kuiba nyaya za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).Hukumu hiyo imetolewa Agosti 25, 2014 katika mahakama hiyo na B. Mashabara baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa hilo la wizi wa nyaya (cables) za kampuni ya TTCL zenye thamani ya shilingi milioni 15.Awali akisomewa shitaka hilo, Muhidin Ndina anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 11, 2013 maeneo ya Boko Katika Wilaya ya Kinondoni kabla ya kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi namba 12/2013.
“…Aliiba nyaya (cables) za thamani ya milioni 15…alitenda kosa hilo Januari 11, 2013 Boko Katika eneo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam…” ilisomeka sehemu ya hukumu ya kesi hiyo.
Uharibifu wa miundombinu ya umma zikiwemo nyaya za simu za Kampuni ya TTCL umekuwa ukishamiri maeneo kadhaa jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kubwa kwa kampuni na usu mbufu kwa wananchi na watumiaji wa huduma za TTCL.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni