Alhamisi, 11 Septemba 2014

PISTOTIUS HAKUKUSUDIA KUUA

Pistorius akisikiliza kesi ya kumuua mpenzi wake kwa maksudi
Jaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda uhalifu alipomuua mpenzi wake Reeva.
Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini amekana kumuua kwa maksudi, akisema alidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Reeva kwa maksudi baada ya wapenzi hao wawili kutofautiana.
Mandishi wa BBC anasema kuwa jaji Thokozile Masipa huenda akachukua hadi Ijumaa kumaliza uamuzi wake.
Pia atakuwa anaangalia kwa makini ukweli wa mashahidi waliotoa ushahidi wao katika kesi hiyo akiwemo Pistorius mwenyewe.
Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
Oscar Pestorius amekana mashitaka ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao ya Valentine mwaka jana.
Mwendesha mashitaka anasisitiza kuwa Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenziwe Reeva baaya ya ugomvi baina yao lakini amejitetea akisema alimpiga risasi kimakosa akidhani mwizi amevamia nyumba yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni