Bertha Lumala na mitandao
Kiungo wa Ivory Coast na Manchester City, Yaya Toure ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika wa Shirikisho l;a Soka barani Afrika (CAF) kwa mwaka wa nne mfululizo.
Kiungo wa Ivory Coast na Manchester City, Yaya Toure ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika wa Shirikisho l;a Soka barani Afrika (CAF) kwa mwaka wa nne mfululizo.
Kiungo huyo ametwaa tena taji huilo baada ya kumbwaga Mnigeria Vincent Enyeama, ambaye alionekana kuwa tishio kwake mwaka huu.
Hata hivyo, taifa lililong’ara zaidi usiku huu wakati wa kutunuku tuzo hizo, ni la Ukanda wa Kaskazini mwa Afrika, Algeria.
Timu
ya Taifa hilo imetangazwa kuwa Timu Bora ya Mwaka, Klabu ya ES Setif
Algeria imetangazwa kuwa Klabu Bora ya Mwaka na kocha swao mkuu,
Kheireddine Madoui ametawazwa Kocha Bora wa Mwaka.
Katika
kung’arisha zaidi tuzo hizo, Kinda wa Algeria, Yacine Brahimi
ametangazwa kuwa ndiye Kinda Mwenye Kipaji Zaidi wa Mwaka Anayechipikia.
Wanawake
wa Nigeria nao hawakuachwa nyuma wakati Falcons hao wakitangazwa Timu
Bora ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka na Asisat Oshoala akaongeza tuzo
nyingine kwa kuibuka Mchezaji Bora Kinda wa Mwaka na Mwanasoka Borav wa
Kike wa Mwaka barani.
Tuzo
ya Refa Bora wa Mwaka imekwenda kwa Papa Bakary Gassama, wakati Tuzo
Mwanasoka Bora wa Mwaka anayecheza ndani ya Afrika imekwenda kwa Firmin
Ndombe Makala
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni