Ijumaa, 9 Januari 2015

MWANAYE JACKIE CHANG JELA KWA BANGI

Jackie chan na mwanawe Jacee Chan
Jacee Chan mwana wa mwana nyota wa filamu Jackie Chan amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kutumia mihadarati.
Jacee Chan mwenye umri wa miaka 32 alikiri kufanya makosa hayo katika mahakama ya wiliaya ya mjini Beijing Dongcheng kwa kuwaficha wengine ili kutumia dawa za kulevya.
Polisi walivamia nyumba yake mnamo mwezi Agosti na kupata gramu 100 za bangi (marijuana).

Kukamatwa kwake kunajiri kufuatia msako wa dawa za kulevya nchini Uchina ambapo watu kadhaa mashuhuri walikamatwa.Jacee Chan na babaake Jackie Chan

Mnamo mwezi Juni mwaka 2014, rais Xi Jinping aliwaagiza polisi kutumia mikakati mikali ili kusitisha utumizi wa mihadarati.

Kukiri kwa mwana wa mcheza filamu mashuhuri nchini Uchina kunatoa ujumbe muhimu kutoka kwa serikali ya Uchina.

Hakuna aliye na kinga nchini Uchina katika msako huo wa dawa za kulevya.

Chan na nyota wa filamu kutoka Taiwan Kai Ko mwenye umri wa miaka 23 walikamatwa pamoja katika nyumba ya Beijing mnamo mwezi Agosti huku polisi wakisema kuwa walipatikana wametumia bangi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni