Msanii
wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto amejikuta mpweke baada ya kupuliziwa
dawa na wezi na kuibiwa vitu vya ndani vyenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 7 usiku wa kuamkia leo. Akizungumza
na mtandao huu kwa masikitiko, Mpoto
amesema wezi hao huenda waliwapulizia dawa hali ambayo ilisababisha kutoshtukia mchezo huo.
amesema wezi hao huenda waliwapulizia dawa hali ambayo ilisababisha kutoshtukia mchezo huo.
Sehemu ya TV na radio
“Yaani
wamesafisha kila kitu,” amesema Mpoto. “Hapa sebuleni hakuna kitu
yaani. Mimi mwenyewe nilikuwepo sema labda ni kwa sababu nyumba kubwa
pia tunahisi labda walitumia dawa kwa sababu sio kawada nikalala hivyo
bila kusikia kinachoendelea. Nahisi walitupulizia dawa za usingizi. Pesa
nyingi sana ni zaidi ya milioni 7, sema tayari suala nimelifikisha
polisi na wanaendelea na upelelezi. Wameiba vitu ni vingi, flati screen,
maredio yaani ni vingi.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni