Jumapili, 24 Julai 2016

Bodi ya Tanzania yafafanua kuhusu Mlima Kilimanjaro

Tanzania


Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania

Bodi ya Utalii Tanzania imetoa taarifa kufafanua kuhusu Mlima Kilimanjaro baada ya shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.

Shirika hilo lilikuwa likiripoti kuhusu kifo cha Guguleth Zulu, raia wa Afrika Kusini, aliyefariki akikwea MlimaKilimanjaro hivi karibuni. Bw Zulu, 38, alikuwa akishuka baada ya kufanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro katika mradi uliopangwa na taasisi ya Nelson Mandela ili fedha itakayopatikana iwanunulie pedi wasichana  nchini Afrika ya Kusini. Ameacha mke aitwaye Letshego na binti wa mwaka mmoja  Lelethu. Bw Zulu alikuwa dereva maarufu wa mbio za magari huko Afrika ya Kusini.
 Gugu Zulu and his wife Letshego
 Bw Zulu na mkewe Letshego wakianza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro
“Tungependa kusahihisha habari za kupotosha zilizochapishwa na Miami Herald, kwamba Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si Kenya,” taarifa iliyotiwa saini na meneja mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ilisema.
Bodi hiyo inasema imeliandikia barua gazeti hilo na kulitaka lichapishe sahihisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni