Jumatatu, 13 Aprili 2015

AJALI NYINGINE YATOKEA SONI LEO, LORI LA MAFUTA LAGONGANA NA BASI LA ABIRIA USO KWA USO

Abiria zaidi ya 50 wamenusurika leo baada ya basi walilokuwa wakisafiria liitwalo Burudani kugongana uso kwa uso na Lori la tenki la mafuta maeneo ya Soni mkoani Tanga. Mashuhuda wamesema hii ajali imetokea baada ya Lori la mafuta kukatika breki na kuvaana na basi hilo uso kwa uso. Habari zinasema hakuna maafa yaliyoripotiwa hadi sasa ila watu kadhaa wamepata majeraha na kukimbizwa hospitali.
Hii ni ajali ya pili ya basi la abiria kutokea leo, ikufuatiwa na ile ya asubuhi maeneo ya Iyovi, Mikumi, jirani na milima ya Udzungwa ambapo imeripotiwa kwamba watu 18 wamepoteza maisha hapo hapo na wengine 10 kujeruhiwa baada ya lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na basi la abiria na yote mawili kushika moto hapo hapo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni