Jumatano, 27 Mei 2015

RAIS KIKWETE AMWAPISHA KATIBU MKUU MAMBO YA NJE NA NAIBU WAKE

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa na naibu wake pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Saudi Arabia katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.


-Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Balozi Liberata Mulamula akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.


Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Balozi Liberata Mulamula akipokea vitendea kazi kutoka kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Balozi Hassan Simba Yahya akila kiapo Mbele ya Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Balozi Hassan Simba Yahya akipokea vitendea kazi kutoka kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.


Balozi mpya wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mh. Hemed Iddi Mgaza akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa miongozo ya kazi(picha na Freddy Maro)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni