Serikali
ya Kenya imemtambua mmoja ya wapiganaji waliohusika katika mauaji ya
chuo kikuu cha Garissa kwamba ni mtoto wa afisa wa serikali.
Mtu huyo sasa ametambulika kama mwana wa kiume wa Chifu wa eneo la Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Alidaiwa kutoweka na ilihofiwa kwamba amesafiri nchini Somalia.
Wizara ya ndani inasema kuwa wapiganaji wote waliuawa siku ya alhamisi.
Washukiwa wengine watano wamakamatwa kufikia sasa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Alshabaab
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni