Taarifa kutoka nchi ya kifalme ya Swaziland zinasema kima cha
fedha katika benki kuu ya nchi hiyo kimebaki dollar laki 8 pekee.
Kamati inayohusika na sera za fedha imesema hela hiyo iliyobaki inaweza kununua bidhaa muhimu kutoka nje ya nchi kwa mahitaji ya mda wa miezi minne pekee.
Kamati inayohusika na sera za fedha imesema hela hiyo iliyobaki inaweza kununua bidhaa muhimu kutoka nje ya nchi kwa mahitaji ya mda wa miezi minne pekee.
Uchumi wa Swaziland umeathirika pakubwa kutokana na kudorora kwa uchumi wa
nchi wanaoitegemea sana jirani zao Afrika kusini ambayo ndio soko kubwa la
bidhaa za Swaziland.
Hata hivyo Patrick Ndzinisa wa benki ya akiba nchini humo ameiambia BBC kuwa
hawana wasiwasi kwani kanuni za kimataifa zanatambua uwezo wa nchi kuagizia
bidhaa zake kwa muda wa hadi miezi mitatu.
Mwaka 2011 Swaziland iliiomba Afrika Kusini msaada wa dharura baada ya kuishiwa na hela.
Mwaka 2011 Swaziland iliiomba Afrika Kusini msaada wa dharura baada ya kuishiwa na hela.
Swaziland ilipiga marufuku vyama vya kisiasa nchini humo tangu 1973 na
imeshtumiwa kwa rekodi yake mbaya ya uvunjaji wa haki za binadamu. Wakereketwa wa
kupigia kampeni mageuzi ya
ki-demokrasia mara nyingi hukamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi kisha kuzuiliwa magerezani.
ki-demokrasia mara nyingi hukamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi kisha kuzuiliwa magerezani.
Mfalme Mswati na familia yake wameshutumiwa kwa ubadhirifu na ufujaji wa fedha
huku wengi wa raia wa Swaziland wakibaki kuwa miongoni mwa maskini zaidi
duniani (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni