Mkwaju
wa penalti uliofungwa na nahodha Wayne Rooney uliisaidia Manchester
United kuichapa Sunderland mabao 2-0 baada ya West Brown kupewa kadi
nyekundu katika kile kilichoonekana kama maonevu.
Rooney alifunga
baada ya mshambuliaji Radamel Falcao kuchezewa visivyo na kusababisha
kutolewa kwa Wes Brown badala ya John Oshea aliyecheza vibaya licha ya
pingamizi kutoka kwa mashabiki.Manchester united iliongeza bao la pili baada ya Rooney kufunga kupitia kichwa baada ya mkwaju wa Adnan Januzaj kupanguliwa na kipa.
Ushindi huo umeimarisha harakati za kilabu hiyo kuwania nafasi nne bora katika ligi hiyo.
Matokeo mengine:
West Ham 1 - 3 Crystal Palace
Burnley 0 - 1 swansea
Newcastle 1 - 0 Aston Villa
Stoke 1 - 0 Hull
West Brom 1 - 0 Southampton
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni