Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
Mbunge wa
kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir, amemtembelea majeruhi wa tukio la
uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino, Yohana Bahati,
aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.
Katika
ziara hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, Mh Shaimar
aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mwanza,
Crecencia Joseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Bayport Financial
Services mkoani Mwanza. Wakiwa
Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana nao alipata fursa
ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Esther ambaye ni mama mzazi wa
hayati Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha yake
pamoja na kulia msiba wa mwanae.
Tukio la
utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi limezidi kushika
kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau, hususan wale
wenye ulemavu wa ngozi wakiamini kuwa serikali imeshindwa kuwapatia
ulinzi wa kutosha.
Akiwa
jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial
Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba kwa ajili
ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili
kati ya watano waliobaki ambao ni albino.
Mbunge wa
kuteuliwa Shaimar Kweigyir kulia akiwa na Mweka Hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdullah Omari wakimpa pole mama mzazi wa Yohana ambaye alikuwa ni mlemavu wa ngozi aliyeuawa hivi karibuni
mkoani Mwanza, huku mama yake akiachwa na majeraha makubwa wakati
wanagombania mtoto katika tukio hilo la kusikitisha.
Katibu wa
Mheshimiwa mbunge, Semeni Kingalu, kulia akipiga picha wakati
walipomtembelea majeruhi Ester Maganiko, ambaye mtoto wake Yohana Bahati
mwenye ulemavu wa ngozi aliuliwa katika tukio hilo la kusikitisha.
Anayefuata ni Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Bugando na Clencencia
Joseph, Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni